MAKALA hii nimeiandika
maalumu kwa watanzania na
wadau wangu wote ,
wanafunzi wa SHULE ZA MSINGI , SEKONDARI, na VYUO wanaopenda
kujifunza LUGHA
YA KIINGEREZA na lugha
nyingne ngeni lengo
ni kuweza KUANDIKA
na KUONGEA kwa
UFASAHA na UMAHIRI.
Limekuwa ni
tatizo kubwa kwa Watanzania wengi na wanafunzi wetu kuanzia ELIMU AWALI, MSINGI,SEKONDARI , VYUO kutoweza
kuongea KIINGEREZA
kwa ufasaha na
umahiri.Hata Lugha ya
KISWAHILI ingawa ni
lugha yetu ya
taifa bado ni
tatizo kwa watanzania
wengi na wanafunzi
kuongea kwa
ufasaha na umahiri ! TATIZO
NI NINI ? UTAKUZAJE UWEZO
WAKO WA LUGHA ? Kujifunza LUGHA yoyote
ni suala
ENDELEVU {long and permanent term
} na
siyo suala la
KUJIFUNZA LUGHA KWA
WIKI TATU TU,
AU MIEZI MITATU
TU ,AU MIEZI
SITA TU ! KAMA MATANGAZO
YA BIASHARA YANAVYOJITANGAZA . “ JIFUNZE LUGHA
YA KIINGEREZA KWA
WIKI TATU “ hii si
kweli ndugu yangu.
LUGHA ni
mtaji , inaweza
kukufanikisha mambo yako
katika maisha ! Ndugu
yangu MTANZANIA kama
wewe ni mbumbumbu
wa Lugha ya
KISWAHILI au KIINGEREZA
utachina au utakwama
katika masuala yako
yanayohitaji UMAHIRI katika
lugha hizo mbili . Kuna umuhimu
sana kwa ndugu
yangu MTANZANIA kuwa
MAHIRI katika kutumia
KISWAHILI au KIINGEREZA
kwa ufasaha na umahiri .
SIRI
ZA KUIKUZA
LUGHA YA KIINGEREZA
---Huwezi kuimiliki
lugha yoyote kama
huitumii.Mtu anaweza kujidai
kuwa kwa vile
ni mswahili na
amezaliwa katika lugha
hii basi anaijua
lugha. Hii si kweli
kabisa ndugu yangu .Kama
ingekuwa hivyo basi
wote tungeweza kutumia
na kuielewa MISAMIATI
na MISEMO yote
ambayo iko katika
lugha yako.Kwanini basi
wengine wakiitumia MISEMO
na MISAMIATI hito
wewe unatoka kappa , ni
kwa sababu huitumii.Kwa
hiyo jambo la
msingi ni kuhakikisha
kuwa unaitumia lugha.
----Kwa
wale wanaojifunza lugha
ya kigeni , jambo
la msingi ni kuhakikisha
kuwa unaitumia ili
uweze kupata uzoefu
na hatimaye kuitumia
kadri unavyotaka.
-----KUITUMIA LUGHA
MAANA YAKE NINI ?
Izungumze au itumie
katika MAANDISHI ; kama ni
lugha ngeni kwako.Kadri
unavyoendelea kuitumia katika
mazungumzo au katika
kuiandika basi unakuwa
na uwezo wa
kuielewa na utahitajika
kupata misamiati mipya.
----Hudhuria katika
mikutano na uhakikishe
unatafuta nafasi ya
kuzungumza. Unapozungumza
katika matukio kama
hayo maana yake
utapaswa kuchagua MANENO/ MISAMIATI na
kuyapanga ili uonekane
unajieleza kwa ufasaha
na kile kinachokusudiwa. UWEZO WA
LUGHA UTAHITAJIKA.
-----Makongamano , au hata
ubishi wa kawaida
mitaani ni nafasi
nzuri kwako wewe
kuitumia ili uweze
kukuza uwezo wako
wa lugha. Na wewe
uingie katika ubishi
halafu uangalie , fanya tathmini , baadaye , kwa nini
ulishindwa au kushinda, kwa nguvu
ya hoja au
kwa hoja ya
nguvu.Kama unamiliki lugha
unaweza KUSHINDA kila
KONGAMANO.
-----Jifunze kutunga
HADITHI au kuzisoma ,
KUTUNGA MASHAIRI.Haya ni
mambo pekee yanayoweza
kukufanya uhitaji uwezo
mkubwa wa lugha
na hazina kubwa
ya MISAMIATI.
UTATUNGAJE MASHAIRI
KAMA MISAMIATI YAKO
NI MICHACHE ?
Aidha ukitunga MASHAIRI
au HADITHI utajikuta
nyakati zote unatafuta
KAMUSI au VITABU
vya MISEMO na
lugha ili uweze
kupata MANENO yanayofaa
katika utunzi wako
kwa ajili hii
LUGHA yako inakua
kwa haraka sana.
Lakini zuri
sana hapa ni
kuwa kadri unavyoendelea kujihusisha
na utunzi wa
MASHAIRI au HADITHI UNATUMIA
MUDA MWINGI KUFIKIRI ,
na jinsi unavyoendelea kushughulika na
mambo hayo, uwezo wako
wa KUFIKIRI NA KUTAFAKARI
nao huongezeka. Ongezeko
la uwezo wako wa
KUFIKIRI ni matokeo
ya kuwa na
UWEZO MKUBWA WA
LUGHA.
----SIKILIZA , Wengine hudhani
KUSIKILIZA sio sehemu
ya kutumia / kujifunza LUGHA.
-----FUNGULIA REDIO, utasikiliza MISEMO
na MISAMIATI mbalimbali
ambayo utahitajika kuielewa
ili uweze kufuatilia kinachoelezwa .Kwa hiyo
basi kadri unvyoendelea kuisikiliza ndivyo
unavyoweza kuielewa vizuri
zaidi. Kwanza
unapoisikiliza lugha ikizungumza
na wenyewe , kwa
mfano , unajifunza MATAMSHI SAHIHI , unajifunza MISEMO
ambayo huwezi kuipata
katika matukio mengine.
Unatakiwa
kuwa mwangalifu katika
kuchagua vipindi , kama unachagua
redio au televisheni ; kuna
TAARIFA YA HABARI
ambayo , hutumia LUGHA RASMI
ili uweze KUJIFUNZA
MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA
REJISTA MBALIMBALI ZA
LUGHA. Lakini chagua
vipindi vya DRAMA
, yaani MICHEZO
YA KUIGIZA. Utajifunza LUGHA
ikizungumzwa katika mazingira
yake halisi--- NATURAL SETTING. Matamshi , mwitiko na
uteuzi wa lugha
unaondana na mazingira.SIKILIZA VIPINDI
VYA DINI , SHULE , SAYANSI ,
UCHAMBUZI na kadhalika
ili uweze kupata
MISAMIATI MBALIMBALI KWA
AJILI YA KUKUSAIDIA.
HITIMISHO
----Kama
unajifunza LUGHA YA
KIGENI , fanya marudio , mazoezi mengi
na soma vitabu
vingi vya hadithi
vya lugha hiyo.
-----Soma
ukiwa na KAMUSI
na tafuta maana
ya neno usilolijua.
----Jizoeze KUSIKILIZA
na KUONGEA ukiwaiga
wajuao ujifunzapo lugha
ya kigeni.
-----Sikiliza MIHADHARA
na REDIO ili
ujifunze kwa wengine
wanavyotamka maneno.
-------Jikumbushe MANENO
magumu kila siku.
------Kila
nafasi unayoipata itumie
kwa kusoma.
------Pambana na
SARUFI za LUGHA
YA KIGENI kikamilifu.
------Jifunze lugha
ya kigeni kwa
kuongea mara kwa
mara.
Asante sana wadau
wangu hasa WANAFUNZI wangu
kwa kusoma makala
hii nzuri sana
kama utaweza mwonyeshe
mwenzako naye asome
apate kuelewa jinsi
ya kukuza
lugha ya kiingereza
na lugha nyingine.
Makala hii imeandikwa
na MWL
JAPHET MASATU , DAR ES
SALAM , TANZANIA ,AFRIKA YA MASHARIKI
anapatikana kwa namba
+255 716 924
136 , EMAIL:
japhetmasatu@yahoo.com
No comments:
Post a Comment